University Students Christian Fellowship – Christian Council of Tanzania (USCF-CCT) TAKWIMU ni jumuiya ya wanafunzi wa Kikristo katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, inayojumuisha wanafunzi kutoka madhehebu mbalimbali ya Kikristo.
Tukiwa chini ya mwavuli wa Christian Council of Tanzania (CCT), tunalenga kuimarisha maisha ya kiroho ya wanafunzi kwa misingi ya Neno la Mungu, maombi, ushirika, na huduma kwa jamii.
USCF CCT TAKWIMU ilianzishwa rasmi katika mwaka wa masomo 2020/2021 ikiwa na wanachama wasiozidi 20, miongoni mwao viongozi walikuwa watano. Kwa hivi sasa tunamshukuru MUNGU kwa maana USCF CCT TAKWIMU ina jumla ya washarika takribani 86 ambao kati yao washarika hai ni takribani 60 tu ambao wanashiriki katika ibada na matukio mbalimbali ya nje na ndani ya Jumuiya yetu na viongozi 21 na ministries mbalimbali ikiwemo Kikundi cha kusifu na kuabudu, IT na Kwaya.
Kukuza na kuimarisha imani ya wanafunzi kupitia mafundisho ya Biblia na ushirika wa Kikristo.
Kuhamasisha maisha ya maombi, utakatifu, na ibada halisi kwa Mungu aliye hai.
Kuwawezesha wanafunzi kuwa viongozi wa kiroho na waadilifu katika jamii.
Kushiriki huduma za kijamii kwa upendo wa Kristo, ikiwemo kusaidia wahitaji na kuhubiri Injili.
Kuwa jumuiya inayojenga kizazi cha wanafunzi wenye imani thabiti kwa Kristo, wakiongozwa na Neno la Mungu katika maisha yao ya kila siku na taaluma zao.
"We serve the living God"