Lift Your Voice to Jesus ni Mkesha wa Kusifu na Kuabudu
Karibu kwenye mkesha wa kipekee wa kusifu na kuabudu kwa jina la “Lift Your Voice to Jesus”!
Huu ni usiku wa kuinua sauti zetu kwa Yesu kupitia nyimbo za sifa, maombi ya nguvu, na kuabudu kwa moyo wote. Tunakualika ujiunge pamoja nasi kwa tukio hili takatifu litakalogusa mioyo na kuinua maisha ya watu kiroho.
Tarehe: 30/5/2025
Muda: Kuanzia saa 3:00 usiku hadi alfajiri
Mahali:
Kauli mbiu: “Lift Your Voice to Jesus"
Tutakuwa na:
• Uimbaji wa kusisimua kutoka kwa waimbaji maarufu na vikundi mbalimbali.
• Neno la Mungu kutoka kwa watumishi wa Bwana waliobarikiwa
• Maombi ya kuinua maisha ya watu binafsi, familia, na taifa.
Mwaliko:
Huu ni mkesha wa wote vijana, watu wazima, familia – kila mtu anayetamani kumkaribia Mungu kwa sifa na kuabudu. Njoo tukutane katika uwepo wa Mungu na tukubali kubadilishwa milele.
Uongozi wa USCF CCT TAKWIMU unapenda kuwataarifu watu wote rasmi mahafali ya awamu ya 4 (2024/2025) yatakayofanyika mnamo tarehe 17 May 2025, AICT CHANGANYIKENI kuanzia saa 3 Asubuhi mpaka saa 9 Mchana, Nyote mnakaribishwa
Alhamisi, tarehe 01 Mei 2025, wanafunzi kutoka matawi yote ya makanisa ya CCT yaliyoko chini ya UDSM CCT CHAPLAINCY walikusanyika kwa pamoja kwenye viwanja vya UDSM Grounds kwa ajili ya USCF BONANZA.
Tukio hili maalum la michezo na burudani lililenga kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanafunzi wa CCT.
🎯 Lengo la Bonanza:
Lengo kuu lilikuwa kuwakutanisha wanafunzi wanaolelewa kiroho na UDSM CCT Chaplaincy kwa ajili ya kufurahi, kushirikiana, na kujenga ushirika wa pamoja kupitia michezo mbalimbali.
🏆 Michezo Ilivyoshindaniwa:
siku ya kesho tutakuwa na ibada yetu maalumu ya shukrani kwa ajili ya mission iliyofanyika Nanyamba pale UDSM, karibuni wote tukamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyotutendea. Nb: Usafiri wa bure(kwenda na kurudi) utakuwepo main gate na gari litaondoka saa 12:30 asubuhi
BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA
Mwenyekiti wa USCF CCT TAKWIMU kwa niaba ya viongozi na washirika wa USCF CCT TAKWIMU anatoa pongezi za dhati kwa Baba Mkubwa wa tawi letu na Mwenyekiti wa USCF Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar ndugu Emmanuel Allen, kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa USCF Taifa katika mkutano wa halmashauri kuu ya taifa uliofanya jijini Mbeya tarehe 19/04/2025.
Kama tawi la Takwimu, tunakupongeza kwa moyo wote na tunakuombea baraka tele, hekima, na nguvu mpya katika kutekeleza majukumu yako mapya. Tunaahidi kuendelea kushirikiana nawe bega kwa bega katika kila hatua ya utumishi wako ili kwa pamoja tuzidi kuujenga mwili wa Kristo.
Hongera sana Baba Mkubwa USCF CCT TAKWIMU!
Hongera mwenyekiti wa USCF mkoa!
Hongera naibu katibu mkuu USCF taifa!
Tunatarajia kuwa na mkutano mkuu wa 12 wa USCF TAIFA ambao huambatana na kongamano la pasaka(EASTER CONFERENCE) na unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 17-20 Aprili kitaifa katika shule ya St.Mary's Mbeya na kiingilio kwa kila mwanachama wa USCF ni 50,000/= hivo tuendelee kujiandaa...
Kuwepo kwa kambi ya maombi itakayo fanyika kuanzia tarehe 04-06 April . Hivyo kila mmoja anakalibishwa kujiunga nasi katika kumtukuza BWANA
Step into the new semester with God! ✨ Join us for a powerful Prayer Service as we seek His guidance and blessings for the journey ahead. Let’s start strong in faith! #NewChapterWithGod
Familia ya USCF CCT TAKWIMU inawatakia wanawake wote Duniani Kheri ya Siku ya Wanawake! Mungu aendelee kuwabariki na kuwainua katika kila hatua ya maisha yenu. Mmeumbwa kwa makusudi maalum—endelea kung'aa ! ✨ HappyWomen'sDay.